Jifunze zaidi kuhusu historia, maadili, na mafanikio ya Endarofta Secondary School
Endarofta Secondary School: Ilianzishwa na wananchi wa Wilaya ya Karatu takribani mwaka 1984. Baada ya miaka kadhaa, wananchi waliamua kuikabidhi shule hiyo kwa Jimbo Katoliki la Mbulu ili liisimamie kwa niaba yao.
Jimbo Katoliki la Mbulu lilikabidhi usimamizi wa shule kwa Shirika la Kikatoliki la Ndugu wa Moyo Safi wa Maria (S.C.I.M. – Brothers Missionaries of Iringa), ambalo limeendelea kuendesha shule hiyo kwa lengo la kutoa elimu bora, malezi yenye maadili mema na kuwajenga wanafunzi katika misingi ya uwajibikaji na utu.
Shule ina uwezo wa kupokea na kuhudumia wanafunzi wapatao 400, wavulana na wasichana, wanaotoka katika maeneo mbalimbali ya Tanzania.
Shule hupata wanafunzi kupitia matangazo yanayotolewa katika mikutano ya wazazi pamoja na mawakala waliopo katika mikoa mbalimbali nchini. Aidha, matokeo mazuri ya wanafunzi katika mitihani ya ndani na ya kitaifa yameifanya shule kujenga sifa nzuri, hali inayowavutia wazazi na walezi wengi kuwaleta watoto wao kusoma Endarofta Secondary School.
Vilevile, wanafunzi wanaohitimu kutoka shule hii wamekuwa wakionyesha maadili mema, uwezo mzuri wa kitaaluma na kujitegemea katika jamii, jambo linalowapa wazazi imani na kuwahamasisha kujiunga na shule hii. Mbinu bora za ufundishaji, ufuatiliaji wa maendeleo ya kitaaluma pamoja na tathmini ya mwenendo na nidhamu ya wanafunzi ni miongoni mwa sababu zinazowafanya wanafunzi wengi kupenda kusoma katika Shule ya Sekondari Endarofta.
Mbali na kutoa elimu bora, shule pia inazingatia malezi ya kiroho na maadili. Wazazi wengi huichagua shule hii kwa sababu inatoa nafasi kwa shughuli za kiroho kufanyika shuleni huku ikiheshimu uhuru wa kila mwanafunzi kuabudu kulingana na imani yake. Ingawa shule inamilikiwa na Kanisa Katoliki, wanafunzi kutoka madhehebu mbalimbali wanaruhusiwa kuabudu kwa uhuru na heshima.
Kwa hiyo, kumleta mwanafunzi katika Shule ya Sekondari Endarofta ni kumhakikishia ukuaji wa kitaaluma, kimaadili na kiroho, hivyo kumwandaa kuwa raia mwema mwenye mchango chanya kwa familia, jamii na taifa.
| 1. Mkuu wa Shule |
Sr.Lucy P Sindano +255692785191 |
| 2. Makamu Mkuu |
philimon mahega 0769881221 |
Jumla ya Walimu: 13